Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro. |
Ujumbe huo ambao gazeti hili limeuona, ulianza kusambazwa juzi,
ukiwataka wajumbe wa kundi la 201 kutoka Zanzibar, kuondoka bungeni ili
theluthi mbili ya Katiba inayopendekezwa isipatikane.
Upigaji wa kura kulingana na masharti ya Ibara ya 37 ya kanuni za
Bunge Maalumu la Katiba, unatarajiwa kuanza Septemba 29 na kukamilika
Oktoba 2 mwaka huu.
Hata hivyo, taarifa nyingine zimedai ujumbe huo unatumwa na baadhi ya
wanaCCM kama mbinu ya kuwakatisha tamaa kundi la 201 wanaoonekana kuwa
na msimamo thabiti ili hatimaye warudi upande wa CCM kwa kuona
wamenyanyapaliwa.
Ujumbe huo unaaminika unaweza kuwa ni sehemu ya propaganda kutoka kwa
baadhi ya wanaCCM kutoka Maskani ya Kisonge Zanzibar ili wajumbe hao
waanze kusalitiana na wale wenye msimamo wajenge chuki na kusalimu amri.
“Tunawaambia wazi wajumbe hao wa kundi la 201 watoke katika Bunge la
Katiba mara moja kabla ya upigaji wa kura vinginevyo hatutawaelewa,”
unasomeka ujumbe huo wa WhatsApp na kuongeza;
“Hatuhitaji wapige kura ya siri wala ya wazi. Tunachohitaji ni
theluthi mbili ya Zanzibar isipatikane kabla hata ya huo upigaji wa
kura”, unasomeka ujumbe huo ambao umeweka picha za baadhi ya wajumbe
baadhi ya wanaCCM kama mbinu ya kuwakatisha tamaa kundi la 201
wanaoonekana kuwa na msimamo thabiti ili hatimaye warudi upande wa CCM
kwa kuona wamenyanyapaliwa.
Ujumbe huo unaaminika unaweza kuwa ni sehemu ya propaganda kutoka kwa
baadhi ya wanaCCM kutoka Maskani ya Kisonge Zanzibar ili wajumbe hao
waanze kusalitiana na wale wenye msimamo wajenge chuki na kusalimu amri.
“Tunawaambia wazi wajumbe hao wa kundi la 201 watoke katika Bunge la
Katiba mara moja kabla ya upigaji wa kura vinginevyo hatutawaelewa,”
unasomeka ujumbe huo wa WhatsApp na kuongeza;
“Hatuhitaji wapige kura ya siri wala ya wazi. Tunachohitaji ni
theluthi mbili ya Zanzibar isipatikane kabla hata ya huo upigaji wa
kura”, unasomeka ujumbe huo ambao umeweka picha za baadhi ya wajumbe.
“Na kama hawakutoka, tunawataka Wazanzibari wawatambue wasaliti hawa,
wawalaani kwa nguvu zote na wawaorodheshe katika daftari la wasaliti wa
Zanzibar kama wenzao akina Balozi Seif Ali Idd (Makamu wa Pili wa Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar),” umesisitiza.
Balozi Idd ambaye ni kada wa CCM, amekuwa akitamka wazi kuunga mkono
mchakato wa Katiba unaoendelea mjini Dodoma, tofauti na baadhi ya
wajumbe kutoka Zanzibar wanaotaka muundo utakaoipa Zanzibar mamlaka
kamili.
Watumaji wa ujumbe huo wanaotumia mtandao wa WhatsApp, wametaka
ujumbe huo usambazwe kwa Wazanzibari wenzao waliopo ndani na nje ya
nchi.
“Linalotusikitisha ni sehemu ya hili kundi la 201 ambao kwa nje
wanaonyesha kuunga mkono madai ya Wazanzibari, lakini kwa ndani
wanaonekana kumbe na wao ni mpini wanalitumikia shoka kuimaliza
Zanzibar,”unadai ujumbe huo.
“Wazanzibari hatuko tayari kupoteza nchi yetu na vizazi vyetu kwa
masilahi ya wanafiki wachache walioamua kwa njaa zao kufakamia mamilioni
ya fedha ili kuiangamiza Zanzibar,” unasomeka ujumbe huo.
Baadhi ya kamati za Bunge zimependekeza Rais wa Zanzibar awe makamu
wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu awe makamu wa pili wa Rais wa muungano.
Hata hivyo, zipo kamati zilizopendekeza kuwapo makamu watatu wa Rais
ambapo Rais wa Zanzibar anapendekezwa awe makamu wa kwanza wa Rais,
mgombea mwenza awe makamu wa pili wa Rais na waziri mkuu awe makamu wa
tatu.
Wajumbe wauona
Hata hivyo, Mjumbe wa Bunge hilo kundi la 201 kutoka Zanzibar, Salma
Said alikiri kuuona ujumbe huo na kwamba hana wasiwasi na
kilichoandikwa katika waraka huo kwa kuwa anaamini wametumia njia yao
ya kidemokrasia ya kujieleza na kutoa maoni yao kama wananchi ingawa
njia waliyotumia siyo sahihi ya kuwaita watu wasaliti.
Alisema wakati huu ni muhimu wa kujenga umoja wa Wazanzibari na siyo kujenga uadui kwa kushutumiana.
Naye Dk Alley Nassoro kutoka kundi hilo alikiri kuuona ujumbe huo na
akasema una lengo la kuwavuruga Wazanzibari wenye msimamo thabiti wa
kutetea masilahi ya Zanzibar katika katiba.
“Baadhi yao walioandaa ujumbe huo tunawafahamu na wamefanya mambo ya
ajabu hata kule Zanzibar na nataka niwaambie Wazanzibar kuwa watu hao
ndiyo wametufikisha hapa tulipo,” alisema.
Dk Alley alisema ujumbe huo unasambazwa na maadui wa Zanzibar na
lengo la kusambaza ni kuwafarakanisha wajumbe wanaotoka visiwani wasiwe
na mshikamano.
Mjumbe mmoja wa Bunge hilo anayetajwa kwenye ujumbe huo alisema ana
matumaini bado ataendelea kuwapo bungeni kwa vile alishiriki mchakato
huo tangu hatua za mwanzo za Bunge.
“Nataka niwahakikishie Wazanzibari kuwa watulie, msimamo wetu ni
thabiti wala hauyumbi. Huo ujumbe ni mbinu tu ya kutaka kutufitinisha na
kutukatisha tamaa. Tumekuja kuwakilisha masilahi ya Zanzibar,” alisema
mjumbe huyo na kuongeza;
“Tukiona ipo haja ya kuondoka na kuliacha Bunge tutafanya hivyo kwa
masilahi ya Zanzibar. Sisi ni watu wazima na tunaamini hizi ni nchi
mbili na zitabaki kuwa mbili na Zanzibar yenye dola kamili.”
Kanuni ya 37 ya Bunge la Katiba, inaeleza ili ibara au sura iweze
kupitishwa na Bunge ni lazima iungwe mkono na theluthi mbili ya wajumbe
wa Tanzania Bara na idadi kama hiyo ya wajumbe wa Zanzibar.
Ni kutokana na hofu ya kutopatikana kwa theluthi mbili, Mwenyekiti wa
Bunge hilo, Samuel Sitta aliwataka mawaziri na naibu mawaziri kuwepo
bungeni kuanzia Septemba 29.
Wito kama huo ameutoa pia kwa wajumbe wa Bunge hilo walioshiriki
mjadala wa Bunge hilo, bila kuhusisha Ukawa waliosusia Bunge hilo tangu
Aprili 16.
Sitta mara zote tangu kuanza kwa Bunge hilo Agosti 5 amekuwa
akiwahakikishia Watanzania kuwa Bunge hilo litakamilisha kazi yake na
kuwapatia Watanzania Katiba bora.
Hata hivyo, habari kutoka kwa baadhi ya wajumbe zinadai kwamba ili
Katiba hiyo iweze kupata theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar, CCM
na washirika wake wanahitaji kura 79.
“Jumla ya Wazanzibar wote ndani ya Bunge ni 217 na theluthi mbili
yake ni wajumbe 144 kwa hiyo ukitoa wajumbe 66 wa Ukawa ambao tayari
hawapo ina maana theluthi mbili ni kura 78,” kilidokeza chanzo hicho.
Hata hivyo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro
amenukuliwa akisema wajumbe wote wa Bunge hilo ni 630 na kati ya hao,
wajumbe waliotoka ni 130, idadi ambayo ni sawa na asilimia 21 ya wajumbe
wote.
“Wajumbe waliobaki ndani ya Bunge ni 500 sawa na asilimia 79 ya
wajumbe wote na idadi hii ni pamoja na wajumbe 189 kutoka kundi la 201
ambao wamebaki bungeni,”alisema.
“Wajumbe wanaotoka Tanzania Bara ni 348 na kati ya hao 125 ni
wanaotoka kundi la 201. Ukitazama takwimu zote hizi, wajumbe wa 201 ni
sehemu ya Bunge hili,” alisema Dk Migiro na kuongeza;
“Kwa Zanzibar wajumbe waliobaki ndani ni 152 na kati ya hao 64
wanatokana na kundi la 201. Waliosusia Bunge kwa pande zote za muungano
hawafikii theluthi moja ya wajumbe waliobaki.”
“Hii ina maana kwa kuzingatia matakwa ya kisheria kuwa uamuzi
upatikane kwa majadiliano na kushawishiana kwa hoja, wajumbe waliobaki
kwa wingi wao wanao uhalali wa kisiasa na kisheria,” alisisitiza Dk
Migiro.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba,
Yahaya Khamis Hamad alisema kuwa hajapata taarifa za kusambaa kwa ujumbe
huo, lakini anaamini mtu anayefanya hivyo ana nia mbaya na Bunge hilo.
“Ungeniambia ni Ukawa ningekuelewa kwa sababu wao ndio wametoka nje
na wanatangaza maandamano nchi nzima…lakini kwa sababu bado sijaouna
siwezi hasa kusema unaweza kuwa na athari kiasi gani kwenye Bunge la
Katiba,” alisema.
No comments:
Post a Comment