Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Samuel Sitta. |
Sitta alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana wakati akielezea
kutoridhishwa kwake na kile alichodai ni namna hukumu ya kesi
iliyofunguliwa na Saed Kubenea inavyopotoshwa na wanaomchukia.
“Kuna baadhi ya vyombo vya habari wananichukia mimi binafsi.
Wasichanganye chuki hizo na mchakato wa Bunge Maalumu,” alisema Sitta na
kuongeza;
“Mimi napokea matusi kila siku. Meseji zisizopungua 50 viongozi wa
Chadema wameweka namba zangu katika tovuti nitukanwe kila siku hilo mimi
niko tayari na mnaniona niko safi tu wala sihangaiki nalo.”
“Lakini sasa Bunge Maalumu ni chombo cha kikatiba, kiko tofauti na
mwenyekiti wake. Huwezi kuliadhibu Bunge Maalumu kwa sababu hupendi sura
ya mwenyekiti wake,” alisema.
Sitta alienda mbali zaidi na kusema, “Kwa hiyo wale wanaoendeleza
hayo mapambano tuendelee na tutaendelea kupambana, lakini kazi ya Bunge
Maalumu itaendelea na ndugu zangu Watanzania mjue tunaandaa Katiba safi
na rafiki kwa wananchi na itapatikana.”
Sitta alisema baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo ya kesi ya Kubenea
dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kumekuwa na tafsiri
alizosema ni potofu.
Baada ya maelezo hayo alimpa ruksa AG, Jaji Frederick Werema kutoa ufafanuzi.
Jaji Werema alisema Mahakama Kuu, katika kutafsiri kifungu cha 25(1)
(2) inakiri kwamba kuna tofauti kati ya kifungu kilichoandikwa Kiswahili
na kile kilichoandikwa Kiingereza.
Alisema Mahakama Kuu katika hukumu hiyo imesema mamlaka ya kuandika
Katiba Mpya ina maana ni mamlaka ya kuandika na kupitisha katiba
inayopendekezwa kwa ajili ya kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya
kupigiwa kura ya maoni.CHANZO: MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment