Ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y-SXP iliruka kutoka Uwanja wa
Ndege wa Mwanza Jumapili saa 1:26 usiku ikielekea Uwanja wa Ndege wa
Jomo Kenyatta (JKIA) Kenya ambako ilitakiwa kutua saa 2:36 usiku.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Paschal
Shelutete alikiri ndege hiyo kuanguka kwenye hifadhi hiyo na walikuwa
katika harakati za kuitafuta.
Mkaguzi Mkuu wa Ajali za Ndege nchini, kutoka Wizara ya Mawasiliano
na Uchukuzi, David Nyamwihura alisema ajali hiyo ilitokea takriban maili
20 kutoka Serengeti, katika eneo la Kogatembe na watu wote watatu
waliokuwamo wamefariki dunia.
Meneja wa Udhibiti wa JKIA, Clever Davor aliliambia gazeti la Daily
Nation la Kenya kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na rada ya uwanja
huo ikiwa imeruka angani urefu wa futi 14,000.
Awali, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya (KCAA) ilitoa taarifa juu
ya kuchelewa kwa ndege hiyo iliyokuwa ikitarajiwa kutua katika uwanja wa
JKIA saa 2 usiku.
Jana asubuhi, Kamanda wa Viwanja vya Ndege wa Kenya (KAPU), Joseph
Ole Tito alithibitisha kupotea kwa ndege hiyo kabla ya kuonekana baadaye
katika Hifadhi ya Serengeti.
Polisi wa Kenya hawakueleza ndege hiyo ya mizigo aina ya Fokker F-27-500 ilikuja nchini kwa shughuli gani.
Ndege zote zinazotoka Kenya kwenda nchi za jirani, huanzia safari
zake katika viwanja vya JKIA, Wilson au Wajir ili kuwa na usimamizi wa
karibu.
MWANANCHI.
MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment