Mjumbe wa Bunge Maalumu, Said Arfi. |
Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Mpanda Kati (Chadema), alilitikisa Bunge
hilo, alipowasilisha maoni ya wajumbe wachache wa Kamati Namba 10
inayoongozwa na Anna Abdallah.
Alisema wajumbe wengi wamependekeza marekebisho ya sura ya saba kwa
kuweka Makamu wa Rais watatu yaani mgombea mwenza, Rais wa Zanzibar na
Waziri Mkuu.
Hata hivyo, alisema wachache wamependekeza sura hiyo kubaki kama
ilivyopendekezwa kwenye Rasimu kwa sababu muundo wa serikali tatu
uliopendekezwa hauhitaji kuwa na makamu wa rais watatu wala ofisi ya
Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa Rasimu hiyo, Ibara ya 70 inasema kutakuwa na Serikali
ya Jamhuri ya Muungano itayokuwa na Rais, makamu na mawaziri wa Jamhuri
ya Muungano.
Tofauti na walio wengi ambao wamependekeza mawaziri na naibu mawaziri
watokane na Bunge, wachache katika kamati hiyo wametaka ibaki kama
ilivyo katika Rasimu ya kuwa mawaziri wasitokane na wabunge.
Alisema mapendekezo hayo yataleta ufanisi zaidi katika utendaji wa mawaziri katika wizara husika.
“Sababu nyingine ni kuondoa uwezekano wa waziri ambaye ni mbunge kupendelea jimbo lake la uchaguzi ili aweze kuchaguliwa tena katika chaguzi zinazofuata,” alisema.
“Sababu nyingine ni kuondoa uwezekano wa waziri ambaye ni mbunge kupendelea jimbo lake la uchaguzi ili aweze kuchaguliwa tena katika chaguzi zinazofuata,” alisema.
Pia alisema wajumbe wengi wameondoa dhana ya Serikali ya Tanganyika
na kufuta mapendekezo yanayoweka utaratibu wa viongozi wa serikali hiyo
kushiriki katika chombo cha uhusiano na uratibu wa Serikali
kinachoanzishwa na Rasimu.
Hata hivyo, alisema wajumbe wachache wamependekeza ibara hizo zibaki
kama zilivyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba kwa sababu maudhui
yaliyowekwa yanakidhi muktadha na majukumu ya chombo husika katika
muundo wa serikali tatu.
Arfi alisema wajumbe wengi walipendekeza kuingizwa kwa sura na sehemu
mpya zilizopendekezwa kuhusu mamlaka ya umma, ardhi, maliasili na
mazingira na sehemu ya Taasisi ya Kuzuia Rushwa katika sura ya 13.
Alifafanua kuwa wajumbe wengi pia walipendekeza sura ya ardhi, maliasili na mazingira.
“Wajumbe wachache hawazikubali sura na ibara mpya zote
zilizopendekezwa kwani zinalenga katika kuongeza mambo ya muungano
katika Rasimu ya Katiba,” alisema.
Katika kamati hiyo, wajumbe wengi wamependekeza kuwapo na uraia wa
nchi zaidi ya moja kwa sababu Watanzania walioko nje ya nchi wangependa
kurudi na kuwekeza nyumbani kwao.
Hata hivyo, alisema wajumbe wachache wamependekeza sura hiyo ibaki
kama ilivyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba kwa sababu kuna hatari
nyingi zinazoambatana na uraia pacha ikiwa ni pamoja na kuhatarisha
usalama wa nchi.CHANZO: MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment