Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi amewapongeza Wabunge na Viongozi wa Mkoa wa Singida kwa
kazi kubwa wanazoendelea kuzifanya za kusimamia miradi ya Kiuchumi na ustawi wa
Jamii ya wananchi wa Mkoa huo.
Amesema usimamizi huo umeufanya Mkoa
huo kuongezeka harakati za maendeleo jambo ambalo wananchi walio wengi
wameonyesha muelekeo mkubwa wa kujitegemea kimaisha.
Balozi Seif alisema hayo wakati wa
hafla fupi ya kukabidhi michango na kupunuza ahadi alizozitoa wakati wa ziara
yake ya hivi karibuni Mkoani Singida aliyoifanya rasmi kuaga kama Mlezi wa Mkoa
huo Kichama.
Akikabidhi michango hiyo kwa Mbunge
wa Jimbo la Singida Mashariki Mh. John Chiligati na Mbunge wa Jimbo la Singida
Magharibi Mh.Alhajj Misanga hapo nyumani kwake Mtaa wa Farahani Mjini Dodoma
Balozi Seif alielezea masikitiko yake kwa kuukosa ukarimu wa Wananchi wa Mkoa
huo aliouzoea wakati wa ulezi wake.
Balozi Seif aliwakumbusha Viongozi
na Wananchi wa Mkoa wa Singida kuendelea kushikamana na yeye atakuwa tayari
kuongeza msukumo wake ili kuona maendeleo ya Kijamii yanazidi kukua na
kustawisha ustawi wa jamii ya wananchi wa Mkoa huo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya
wananchi wa Mkoa wa Singida Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mh. John
Chiligati alisema Balozi Seif Ali Iddi alifanya kazi kubwa iliyoleta
mshikamanio wakati akiwa Mlezi wa Mkoa huo wa Singida.
Mh. Chiligati alisema Balozi Seif
amekiacha Chama cha Mapinduzi imara ndani ya Mkoa wa Singida na wakaahidi
kwamba malezi mema aliyoyaacha watajitahidi kuyaendeleza ipasavyo.
“ Ukweli tumesikitika kumkosa mlezi
muadilifu aliyetuachia majonzi kutokana na uitendaji wake. Lakini hata hivyo
tumemuwekea milango wazi awe huru kushauri na kusaidia harakati za maendeleo ya
wananchi wa Singida “. Alisema Mh. John Chiligati.
Mbunge huyo wa Jimbo la Singida
Masharik pia limpongeza na kumshukuru Mke wa Mlezi huyo Mstaafu wa Mkoa wa
Singida Mama Asha Suleiman Iddi kwa msimamo wake wa kusimamia ilani na sera za
Chama cha Mapinduzi Kivitendo.
Mh. Chiligati alimuelezea Mama Asha
kuwa ni jasiri kutokana nay eye pamoja na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama
Mwanamwema Shein kuuongoza Umoja wa wake wa Wabunge na Wawakilishi wa CCM
Zanzibar ambao umeleta mafanikio makubwa hasa kwa akina mama na watoto.
Balozi Seif katika hafla hiyo fupi
alikabidhi mchango wa shilingi Milioni moja na laki Tano kwa ajili ya ununuzi
wa mabati ya kuezekea jengo la Mabara ya Skuli ya Sekondari ya Chikuyu iliyopo
Wilaya ya Manyoni,shilingi 1,000,000/- za kununulia matofali kwa uendelezaji wa
Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mtunduru pamoja na shilingi 1,000,000/- kwa ajili
ya Madrasa ya Muzdalifa iliyopo Ilongero.
Balozi Seif pia akakabidhi zawadi za
Seti moja moja za Jezi na mipira minne kwa timu za soka na mpira wa pete wa
Skuli ya Iyumbu pamoja na skuli ya msingi ya Ilongero.
No comments:
Post a Comment