Wakili wa Said Kubenea, Peter Kibatara (kushoto) akijadiliana jambo na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam. |
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi la Serikali dhidi ya shauri lililofunguliwa na Wakili Peter Kibatala kwa niaba ya Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea.
Shauri litakalosikilizwa ni la kuomba tafsiri ya kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na tamko kuhusu mamlaka ya Bunge la Katiba pamoja na Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Kubenea, anaiomba Mahakama itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba kwa kuzingatia kifungu cha 25 (1) na (2) cha Sheria ya Marekebisho ya Katiba Namba 83 ya mwaka 2011.
Pia, anaiomba Mahakama itamke kama Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Jopo la majaji watatu, wakiongozwa na Augustine Mwarija, Dk. Fauz Twaib na Aloyisius Mujulizi, litaanza kusikiliza kesi hiyo ya msingi leo.
Awali, Mahakama hiyo ilitupilia mbali maombi ya kusimamisha kwa muda vikao vya Bunge vinavyoendelea Dodoma.
Kesi hiyo yenye namba 28 ya mwaka 2014, ilifunguliwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
No comments:
Post a Comment