Silaha. |
Majambazi hao baada ya kuvamia kituo hicho, waliua askari wawili, kujeruhi wawili na kupora silaha mbalimbali.
Akizungumza jana kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya mifugo uliyofanyika mkoa hapa, na kukutanisha pia wizara tano mtambuka zinazohusiana katika utendaji, IGP Mangu alisema baada ya kumnasa mtuhumiwa huyo, alionyesha alipoziweka silaha sita pamoja na mabomu ya machozi waliyokuwa wamepora katika kituo hicho.
Hata hivyo, alisema ujambazi huo unaendelea kutokana na mapori makubwa yenye wafugaji ambao wamevamia, hivyo kushindwa kufanya operesheni ya kukamata majambazi na wahalifu.
Alisema maeneo makubwa yana mapori ya hifadhi, ambayo wafugaji wamekuwa wakiyatumia hivyo jeshi la polisi likipitisha msako, wafugaji na wahalifu wanakuwa wamechanganyika.
“Kuna mapori makubwa mengi katika mikoa hii… ambayo ama kwa hakika wahalifu wamekuwa wakijificha huko, sasa wafugaji wanavamia, hao pia wanafanya uhalifu wanateka watu wanawafanyia watu vibaya lakini tunashindwa kujua sasa yupi mhalifu na yupi mfugaji,” alisema IGP Mangu.
Alibainisha kuwa, kwa sasa Jeshi la Polisi halina msamaha tena kwa mfugaji yeyote atakayeingia katika pori la hifadhi, atakamatwa na kuchukuliwa hatua.
Alisema wizara zilizopo ambazo zimekutana pamoja kuzungumzia sekta ya mifugo, zishirikiane na jeshi la polisi kuhakikisha wanazuia ufugaji wa kuhama hama ambao umekithiri na unaharibu mazingira.
Pia, aliwataka wafugaji kufuga kisasa, kwani kufuga kienyeji kunakuwa furaha kwa mfugaji huyo lakini kero kubwa kwa mwananchi mwingine.
Naye Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kamani, aliwataka wafugaji wote nchini kufuata sheria ili kuepuka kukamatwa na kutozwa faini, jambo ambalo linawarudisha nyuma.
Aliwataka kufuga kisasa kwa kuotesha nyasi na kulishia mifugo yao, badala kupeleka mifugo katika maeneo yaliyotengwa ya hifadhi za taifa.
Mkutano wa wadau wa mifugo umehusisha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Tamisemi, Kilimo, IGP Mangu na wakuu wa wilaya na mikoa mbalimbali.
No comments:
Post a Comment