Na Madina Issa
RAIA wa Poland mwenye umri wa miaka
31 (jina linahifadhiwa), anadaiwa kubakwa na mfanyakazi wake wa ndani.
Tukio hilo limetokea alfajiri ya
Septemba 14 katika kijiji cha Jambiaji Kibigija wilaya ya kusini Unguja, ambapo
mtuhumiwa ni mfanyakazi wa jikoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kusini Unguja, Juma Sadi Khamis, amethibitisha kutokea tukio hilo na kumtaja
mtuhumiwa kuwa ni Kantenina Alois Jakob (34) mkaazi wa kijiji hicho.
Alisema kabla ya tukio hilo,
mwanamke huyo aligombana na mume wake na kuamua kwenda kulala kwenye nyumba
nyengine.
“Siku ya tukio mwanamke huyu
aligombana na mume wake baada ya kurudi nyumbani wakitoka klabu ya starehe na
kwenda kulala nyumba nyengine, huku mume akiendelea kulala kwenye yumba yao ya
kawaida,” alisema.
Alisema mume alimjulisha mfanyakazi
wao kuhusu tukio hilo, lakini ilipofika usiku mtuhumiwa alikwenda kwenye nyumba
aliyolala bosi wake wa kike na kuingia ndani atakatekeleza kitendo hicho.
“Alikuta mlango uko wazi, akaingia
ndani na akafanya kitendo hicho na kumsababishia maumivu makali na sasa
mtuhumiwa anashikiliwa kwa upelelezi,” alisema.
Alisema mwanamke huyo alimefikishwa
hospitali ya Makunduchi kwa matibabu na baadae kuhamishiwa hospitali kuu ya
Mnazimmoja.
Daktari wa kitengo cha mkono kwa
mkono hospitali kuu ya Mnazimmoja, Salum Omar Mbarouk, alikiri kumpokea
mwanamke huyo na kusema alipomfanyia uchunguzi aligundua michubuko kwenye
sehemu zake za siri na mikwaruzo ya kucha kwenye mapaja na kifuani.
Aidha alisema mtuhumiwa nae alifanyiwa
uchunguzi kwa kupimwa HIV na baadae kukabidhiwa jeshi la polisi kuendelea na
upelelezi.
Alitoa wito kwa wananchi
wanaofanyiwa vitendo vya udhalilishaji kuwahi kufika kituoni hapo ili kupatiwa
matibabu pamoja kutunza ushahidi utakaotumiwa wakati watuhumiwa wanapofikishwa
mahakamani,
Zanzinews.
No comments:
Post a Comment