Wakili wa Said Kubenea, Peter Kibatara (kushoto) akijadiliana jambo na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam. |
Uamuzi huo ulifikiwa jana baada ya kumaliza kusikiliza hoja za pande
zote, upande wa mdai (Kubenea) na upande wa mdaiwa (Serikali).
Katika kesi hiyo namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama
hiyo itoe tafsiri sahihi ya kifungu hicho kuhusu mamlaka ya Bunge hilo
na pia itamke iwapo lina mamlaka ya kuacha maudhui ya Rasimu ya Katiba
iliyowasilishwa bungeni.
Kabla ya mahakama kufikia hatua hiyo ya kupanga tarehe ya kutoa
hukumu yake kwanza, kuliibuka mvutano wa kisheria kuhusu utata wa
tafsiri ya kifungu cha 25(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka
2011 katika lugha mbili zilizotumika kuandika sheria hiyo.
Utata huo unatokana na tofauti ya tafsiri ya kifungu kinachohojiwa
katika toleo la lugha ya Kiingereza na la Kiswahili. Utata huo
uliibuliwa na Jaji Aloysius Mujulizi. Majaji wengine katika jopo hilo ni
Augustine Mwarija na Dk Fauz Twaib.
Baada ya mabishano makali mahakama iliwataka mawakili wa pande zote
kufika mahakamani kesho kwa ajili ya kusikiliza hukumu endapo itakuwa
imekamilika na iwapo itakuwa bado, basi mahakama itatoa maelekezo
mengine.
No comments:
Post a Comment