Bunge hilo awali lilipangwa kumalizika Oktoba 31. Waliojiunga na upatu huu, wamelenga kupata fedha kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu mwakani.
Taarifa za uhakika zilizoifikia NIPASHE, zinasema upatu huo unaendeshwa kwa makundi ya watu sita, ambapo kila mjumbe huchangia Shilingi milioni tatu na mjumbe mmoja kupokea Sh. milioni 18 kwa wiki.
Chanzo chetu cha habari kilisema kuwa lengo la mchezo huo ni kupata fedha za kujiandaa kugombea majimbo kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mmoja wa wajumbe kutoka kundi la 201 ambaye hayumo kwenye mchezo huo, aliiambia NIPASHE kuwa wanaojihusisha na mchezo huo ni kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Zanzibar, Mbeya, Shinyanga na Arusha.
Alisema mchezo huo ulianza mara baada ya Bunge hilo kuanza Agosti 4, mwaka huu, ambapo kila kundi liliweka utaratibu wake maalum wa kupeana pesa.
“Mimi nilishawishiwa lakini niliona hakuna manufaa niliamua kukataa, lakini wenzangu hadi leo wanaendelea na mchezo wa upatu kwa misingi ya kupata urahisi wa kwenda kugombea ubunge mwakani,” alisema mjumbe huyo.
Mjumbe mwingine ambaye hakutaka jina lake liandikwe, alisema suala hilo bado linafukuta chini kwa chini, linaweza kuibuka wakati wowote endapo watu wanaoongoza upatu huo wakashindwa kuchukua hatua ya kutatua tatizo hilo.
“Unajua tulikuwa hatujui kama Rais Kikwete, atakubaliana na Ukawa na kufupisha muda wa bunge, tunavyoongea na wewe baadhi yetu tufanya utaratibu wa kuchukua pesa zetu kwa muda uliopo, tumechanganyikiwa,” aliongeza mjumbe mwingine.
Katika suala la wajumbe hao wa 201, kuwania zafasi za ubunge, imeelezwa imeongeza kasi ya uchangiaji katika mjadala ndani ya Bunge hilo ili kuwafanya waonekane na wananchi.
Kutokana na hali hiyo, majina yanayowasilishwa mbele ya kiti cha bunge hilo yamekuwa mengi kiasi cha kutoa changamoto kubwa.
Hata hivyo, alipotafutwa Katibu wa Bunge Maalum la Katiba, Yahya Khamis Hamad, alisema jambo hilo halifahamu na hawezi kulizungumzia.
Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hilar, akizungumzia suala hilo alisema hatua ya wajumbe hao kuhamasika kugombea kwenye majimbo ni suala la kidemokrasia, hivyo hakuna kipingamizi.
Alisema kama kutatokea mbunge ambaye ataona kama kusalitiwa, basi atakuwa na tatizo kwenye jimbo lake, hivyo wakati uliobaki anatakiwa kujirekebisha.
“Kwangu mimi naona ni jambo la kawaida, muhimu kwetu wajumbe wa kundi hili la 201 wametupa changamoto na kama wabunge tukubali kukabiliana nao,” alisema.
No comments:
Post a Comment