Jeshi la Polisi likiendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma. |
Wakati wote kumekuwa na simulizi ya ulinzi ulioimarishwa katika
viwanja vya Bunge la Katiba tangu kuanza kwake Februari 18, mwaka huu,
ingawa kwa sasa umeongezeka mara dufu.
Tangu Chadema walipotangaza nia yao ya kufanya maandamano ya kupinga
kuendelea kwa Bunge hilo, vyombo vya ulinzi viliweka mkakati wa
kuhakikisha hakuna mtu anayeweza kupenya na kulifikia jengo hilo bila
kibali maalumu.
Jana, Polisi waliongeza umbali wa ulinzi katika kulifikia jengo la
Bunge na hakuna gari wala mtu aliyeweza kuwapita polisi hao bila ya
kukaguliwa na kuulizwa vibali.
Kwa muktadha huo, ili kufikia sehemu ya ukumbi wa Bunge, kulimlazimu
mtu kama mwandishi wa Habari kuvuka vizuizi vitatu ndipo afike sehemu ya
kufanyia kazi zake.CHANZO: MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment