Saturday, 2 April 2016

Watuhumiwa wanne wa milipuko watiwa mbaroni Zanzibar

Kamishna Msaidizi Naibu Mkurugenzi Upepelezi na Makosa ya Jinai Salum Msangi
Jeshi la Polisi Zanzibar linawashikilia watuhumiwa wanne wa usambazaji uratibu na ulipuaji wa milipuko ambayo imetokea kabla ya uchaguzi wa marejeo katika maeneo mbalimbali visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi Naibu Mkurugenzi Upepelezi na Makosa ya Jinai Salum Msangi, watuhumiwa hao ambao wanaendelea kuhojiwa wamekiri kuhusika na kutaja maeneo ambayo waliyalenga katika mapango wao.

Maeneo hayo ni pamoja na nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, nyumba ya Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na nyumba ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai.

Akitowa taarifa mbele ya wanahabari  Naibu Mkurugenzi upelelezi na makosa ya jinai Salum Msangi amesema jeshi limeshakamata mabomu matano huku akisema kuwa wahusika wote waliokamatwa ni wafuasi na viongozi wa chama cha wananchi CUF.

Aidha amesema mtengenezaji wa mabomu hayo ya kienyeji yenye madhara makubwa wameshamtambuwa na kumtaka ajisalimishe kabla mkono wa dola haujamshika  huku akiwaasa viongozi wa CUF waache kuchochoa uhalifu.

Amewataka wananchi na wapenda amani wote kuwafichuwa kila anaeonekana na viashiria vya kufanya uhalifu wa aina yeyote.

CHANZO: STAR TV

No comments:

Post a Comment