George Fellowes ni mwanafunzi wa
chuo kikuu mwenye umri wa miaka 22 na anaamni kwamba hata yeye hupatwa na
''hedhi ya kiume''.
Anasema kuwa ni rafiki wa karibu wa
Amber May Ellis jirani yake na hivyobasi hupata uchungu wa hedhi kila mwezi
rafikiye anapopata hedhi.
Uchungu huo anasema huwa mkali hadi
kulazimika kuchukua likizo ya kuwa mgonjwa.Akizungumza na Newsbeat,George
anaelezea:Nadhani ni swala la kifikra kwa sababu sisi ni marafiki wa karibu
sana na tuna hisia sawa.
Katika kipindi cha miaka mitatu
iliopita anasema kuwa amekuwa akipata uchungu wa hedhi na ishara hizo ni sawa
na zile za wanawake.
Ninapata uchungu chini ya tumbo
langu pamoja na katika kinena.Huwa nahisi vibaya na kuwa na hasira na marafiki
wangu wengi.Pia huwa na hisia zenye mhemuko.
''Huwa sipendi kulia wakati huo
lakini huwa na hasira nyingi.Kuna kitu kimoja kisichomuathiri George hatahivyo.
Sidhani kwamba wanaume wanaweza
kupata hedhi bila kutokwa na damu'',anasema.
''Wakati unapokuwa rafiki wa karibu
na mtu nadhani homoni zenu hufanana''.
George anaelezea kwamba wakati
alipoanza kupata uchungu miaka mitatu iliopita alitaka ushauri wa daktari wake.
Lakini hakukuwa na maelezo hivyobasi
alipewa dawa za kumaliza maumivu ya kinena.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment