Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli ameahirisha shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambyo yalikuwa yafanyike tarehe 26 April mwaka huu.
Taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Nd, Gerson Msigwa imeeleza kuwa siku hiyo itakuwa ya mapumziko kama kawauda na watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama katika shughuli zao binafsi.
Kufuatia kuahirishwa kwa shamra shamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa pesa zilizo tengwa kugharamia shughuli hiyo zielekezwe katika ujenzi wa barabra ya Uwanja wa Ndenge jijini Mwanza.
"Fedha zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kugharamia vinywaji, vyakula, Gwaride, Halaiki, Burudani na hafla ya usiku amabazo ni zaidi ya shilingi bilioni mbili zitumike kuanzisha upanuzi wa barabara ya 'Mwanza Airport' katika eneo limnaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza." ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha amesema kuwa barabara hiyo inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na kero ya msongamano mkubwa wa magari amabao unaathiri shughuli za kila siku za wananchi.
Tangu kuingia madarakani kwa Raia Magufuli mwishoni mwa maka jana, hii ni mara ya pili kuakhirisha serehe za kitaifa baada ya zile za Uhuru wa Tanganyika ambazo alielekeza siku hiyo itumike kwa kufanya usafi wa mazingira mnamo tarehe 9 Disemba mwaka jana.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeasisi mnamo mwaka 1964 chini ya Mwalimu Julius K Nyerere aliyekuwa Rais wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Sheikh Abeid Amani Karume aliyekuwa Rais wa iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambapo tarehe 26 April mwaka huu unatimiza miaka 52 tokea kuasisiwa kwake.
No comments:
Post a Comment