Bunge la Afrika Kusini. |
Awali naibu spika alikuwa amewataka wabunge wapaze sauti hadharani kuhusu iwapo alikuwa anaunga mkono kura ya kutokuwa na imani au la.
Hata hivyo upinzani ulishinikiza kura hiyo iendeshwe kwa njia halisi sawa na kura zingine.
Wachanganuzi wa maswala ya kisiasa nchini Afrika kusini walikuwa wanatarajia matokeo hayo kutokana na idadi kubwa ya wabunge wa chama tawala cha ANC.
Bunge la Afrika Kusini liliamua kusikiza na kujadili hoja ya kumng'oa rais Jacob Zuma kufuatia shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani.
Spika wa bunge la Afrika Kusini bi Baleka Mbete, alikubali hoja hiyo ijadiliwe kufuatia mahakama ya juu ya Afrika Kusini kumpata rais Zuma na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka yake.
Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema kilienda mahakamani kikitaka rais Zuma ashurutishwe kulipa fedha zilizotumika kinyume cha sheria kufanya ukarabati katika makazi yake ya Nkandla.
Upinzani uliwasilisha kesi mahakamani baada ya bwana Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka 2014 kuwa alinufaika kutokana na ukarabati wa nyumba yake na kwamba alistahili kulipa pesa zilizotumiwa.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment