Thursday, 4 September 2014
Dk Shein: Tanzania inaunga mkono mpango wa hifadhi ya mazingira wa visiwa vya ukanda wa magharibi wa bahari ya hindi
Akizungumza katika uzinduzi wa mpango huo uliofanyika jana mjini Apia katika visiwa vya Samoa, Rais wa Zanzibar na Mwenyeiti wa Barala la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alisema mpango huo unatoa fursa kwa washiriki kufanyakazi kwa pamoja katika kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na mabadilko ya tabianchi.
“changamoto tunazokabiliana nazo zinafanana na ni sahihi kufanyakazi pamoja kukabiliana nazo. Mpango huu ni wa manufaa sana katika eneo letu” alieleza Dk. Shein na kusisitiza kuwa katika hali hiyo “Tanzania tunauunga mkono kikamilifu”
Katika hotuba yake fupi kwenye hafla hiyo Dk. Shein ambaye yupo hapa pia kumuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa unaoendelea sasa alieleza pia umuhimu wa taasisi za kikanda za maeneo ya visiwa kusimama pamoja na kuwa na msimamo mmoja katika mkutano huo ili uweze kuweka msingi madhubuti wa ushikiriano.
Alibainisha kuwa kufanyika kwa uzinduzi wa mpango huo sambamba na mkutano wa nchi za visiwa wenye kuhimiza maendeleo endelevu ni fursa nyingine kwa nchi wanachama wa mpango huo kufanya masuala yao kueleweka miongoni mwa jumuiya ya kimataifa.
Aliongeza kuwa ushiriki wa wadau wengi katika uzinduzi wa mpango huo ni ishana kuwa mpango huo umepokelewa vyema na wadau hao wako tayari kushirikiana na wanachama kutekeleza malengo ya mpango huo.
Hata hivyo alihimiza mpango huo kuchukua hatua za haraka kutekeleza programu zake za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa muda hausubiri hivyo kila wakitekeleza mapema itakuwa ni manufaa zaidi kwa uhai na ustawi wa ukanda wa magharibi wa bahari ya Hindi.
Katika hotuba yake hiyo Dk. Shein pia aliwasilisha salamu za Rais Kikwete kwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi ambayo ilihudhiriwa na viongozi mbalimbali wa nchi za visiwa kutoka pande zote za dunia.
Miongoni mwa viongozi walihudhuria na kupata fursa ya kuzungumza ni pamoja na Rais wa Visiwa vya Palau Tommy E. Remengesau Jr., Rais wa Serikali ya Shirikisho la Visiwa vya Micronesia Emanuel Mori na Rais wa visiwa vya Marshall Christopher Loeak.
Wengine ni Waziri Mkuu wa Samoa Tuilaepa Lupesoliai Sailele Malielegaoi, Waziri Mkuu wa Grenada Dr. Keith Mitchell, Waziri wa Mambo ya Nje wa Seychelles Jean-Paul na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Lapo Pistelli.
Mpango wa Magharibi ya Bahari ya Hindi wa Changamoto za Ukanda wa Pwani na Mabadiliko ya Tabianchi ni mkakati mpya wa kiutekelezaji miongoni mwa nchi za visiwa vidogo vya eneo la ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi katika kusimamia malengo ya maendeleo endelevu kwa nchi hizo.
Malengo makubwa Mapango huo yamejikita zaidi katika uhifadhi na usimamizi wa pamoja wa mazingira ya visiwa, fukwe, na bahari zake pamoja na mabadiliko ya tabianchi.
Visiwa vinavyoshiriki mpango huu ni pamoja na Shelisheli, Comoro, Mauritius, Reunion na Zanzibar.
Hatima ya Bunge la Katiba mikononi mwa JK
![]() | |
| Rais Jakaya Mrisho Kikwete. |
Hiyo ni kutokana na muda uliopangwa kwenye ratiba ya bunge hilo kuzua
utata wa kisheria na kuwapo uwezekano wa mwingiliano na Bunge la
Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi (BLW), Zanzibar.
Ratiba ya Bunge Maalumu la Katiba inaonyesha kuwa limepanga
kuhitimisha vikao vyake mwishoni mwa Oktoba, tofauti na tarehe
iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete Julai 28, mwaka huu ambayo
ilitangazwa katika Gazeti la Serikali (GN) namba 254 la Agosti Mosi.
Tangazo la Rais linaonyesha kuwa awamu ya pili ya Bunge Maalumu
ingeanza Agosti 5, 2014 na kumalizika Oktoba 4, lakini ratiba ya Bunge
hilo inaonyesha kuwa litamalizika Oktoba 31, siku ambayo mwenyekiti wa
Bunge hilo atakabidhi kwa Rais Katiba inayopendekezwa.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa hadi sasa Serikali
bado haijatoa tangazo (GN) lingine kuongeza muda hadi mwishoni mwa
Oktoba kama alivyosema Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta wakati
akitoa ufafanuzi wa siku 60 zilizotengwa kwa ajili ya Bunge hilo, Agosti
5 mwaka huu.
Sitta alisema kwa kadiri ya tafsiri, siku za kazi ni Jumatatu hadi
Ijumaa ambazo wajumbe wanapaswa kufanya kazi na kwamba Jumamosi na
Jumapili siyo sehemu ya siku 60 zilizoongezwa na Rais.
Hata hivyo, Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alisema hadi
sasa hawajapata maelekezo ya ziada kutoka serikalini ambako waliandika
barua ya kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu suala hilo.
“Tulimwandikia barua, Katibu Mkuu Kiongozi (Ombeni Sefue) kuomba
ufafanuzi wa siku hizo kama ambavyo sisi tungependa iwe, lakini hadi
sasa bado hatujajibiwa lakini bado siku zipo nadhani tutajibiwa tu
wakati mwafaka,” alisema Hamad ambaye pia ni Katibu wa Baraza la
Wawakilishi.
Sefue alikiri ofisi yake kupokea barua kutoka Bunge Maalumu ikiomba
ufafanuzi ambao ungeliwezesha kuongeza siku kwa lengo la kukamilisha
kazi ya kujadili na kuandika Katiba inayopendekezwa na kwamba maombi yao
bado yanafanyiwa kazi.
“Bado tuna muda wa kutosha tu, ni kweli tulishayapokea maombi ya
Bunge Maalumu kuhusu suala hilo na Mheshimiwa Rais akikamilisha kazi
yake watajulishwa tu,”alisema Sefue.
Utata wa kisheria
Licha ya ahadi iliyotolewa na Sitta ni dhahiri kwamba suala hilo lina
utata wa kisheria kutokana na kauli iliyowahi kutolewa na Mwanasheria
wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema wakati akitoa ufafanuzi wa maana
ya siku 70 ambazo Bunge lilikaa mara ya kwanza.
Baada ya kusoma hati ya Rais ya kuitishwa kwa Bunge hilo, Februari
mwaka huu, Jaji Werema alisema siku 70 zilizotolewa kwa mujibu wa
tangazo la Serikali ni za kikalenda na siyo siku za kazi kwa sababu
wajumbe wa Bunge Maalumu siyo watumishi wa kuajiriwa.
Maelezo ya Jaji Werema yalitokana na swali lililoulizwa na Mjumbe wa
Bunge Maalumu, Ezekiah Oluoch ambaye alitaka ufafanuzi huo kutokana na
siku zilizotengwa kuonekana kwamba ni chache na zisingetosha kukamilisha
kazi ya kutunga Katiba.
Kauli ya Jaji Werema haijawahi kutenguliwa na Mahakama au yeye
mwenyewe na kwa msingi huo, kwenda kinyume chake ni kuvunja Sheria ya
Kazi na Majukumu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sura ya 268 ya 2005.
Vifungu vya 22 (1) na (2) vya sheria hiyo vinazungumzia ushauri wa
kisheria wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu suala lolote analotakiwa
kulitolea ufafanuzi, wakati Kifungu cha 23 (1) kinasema ushauri huo
unabaki kuwa msimamo wa Serikali katika suala husika, vinginevyo
ubatilishwe ama na Mahakama au na AG mwenyewe katika utekelezaji wa
wajibu wake.
Jana katika maelezo yake, Katibu Mkuu Kiongozi, Sefue alisema Jaji
Werema alikuwa sahihi katika tafsiri aliyoitoa kuhusu siku zilizotolewa
na Rais wakati wa awamu ya kwanza ya Bunge Maalumu.
“Jaji Werema yuko sahihi kabisa, kwa hiyo hata Rais atakapokuwa
akitoa majibu ya maombi yaliyofikishwa kwake kuhusu nyongeza ya siku
atazingatia sheria za nchi,” alisema.
Bunge la Muungano na BLW
Mgogoro mwingine unaojitokeza ni ratiba za vikao vya Bunge la Muungano ambalo limepangwa kuanza Novemba 4, 2014 na Baraza la Wawakilishi ambalo limepangwa kukutana kuanzia Oktoba 22, mwaka huu.
Mgogoro mwingine unaojitokeza ni ratiba za vikao vya Bunge la Muungano ambalo limepangwa kuanza Novemba 4, 2014 na Baraza la Wawakilishi ambalo limepangwa kukutana kuanzia Oktoba 22, mwaka huu.
Kwa kawaida, vikao vya Bunge hutanguliwa na wiki mbili za vikao vya
kamati za kudumu na ikiwa ratiba itabaki kama ilivyo, basi vitaingiliana
na vikao vya Bunge Maalumu ambalo ratiba yake imepangwa kuendelea hadi
Oktoba 31, mwaka huu.
Katibu wa Bunge la Muungano, Dk Thomas Kashililah alisema vikao vya
Kamati za Bunge hilo vinatarajiwa kuanza Oktoba 13, mwaka huu kutokana
na kuwapo kwa miswada mingi ya Serikali inayopaswa kufanyiwa kazi.
“Tuna miswada ya Serikali kama 12 hivi ambayo mingine imekaa muda
mrefu, kwa hiyo kamati zetu nyingi zinapaswa kukutana mapema ili
kuifanyia kazi vinginevyo tutakwama,” alisema Dk Kashililah ambaye pia
ni Naibu Katibu wa Bunge Maalumu.
Alipoulizwa kuhusu mwingiliano wa ratiba baina ya taasisi hizo mbili
ambazo yeye ni mtendaji wake, Dk Kashililah alisema suala hilo
litatafutiwa ufumbuzi kabla ya muda huo kuwadia.
“Nadhani wakati tunafikiria suala la muda wa Bunge la Katiba,
hatukufikiria ratiba hizi nyingine, kwa hiyo ni dhahiri kwamba pengine
tutalazimika kuangalia jinsi ya kutoka hapo,” alisema.
Naibu Spika wa Bunge la Muungano, Job Ndugai mwishoni mwa wiki
iliyopita alisema kwa jinsi ratiba ya Bunge Maalumu ilivyopangwa lazima
itaingilia shughuli za Bunge la Muungano, hivyo uamuzi unapaswa ufanywe
ili kuepusha mgongano huo.
“Sisi tumeishaliona hilo kwamba ni changamoto, tulikuwa tukijaribu
kujadiliana kuona kama baadhi ya vikao vya kamati vinaweza kuanza mapema
hapa Dodoma, lakini uamuzi bado haujafanyika,” alisema Ndugai.
Naye Hamad alikiri kwamba kalenda ya vikao vya Baraza la Wawakilishi
inaingiliana na ratiba ya Bunge Maalumu na kwamba wanafikiria jinsi ya
kuondoa kasoro hiyo.
“Kuna njia nyingi za kuondoka hapo, pengine tunaweza kumwomba Rais
asogeze mbele vikao vya Baraza la Wawakilishi kwa wiki mbili, maana hiyo
inaruhusiwa kwa mujibu wa Katiba. Hata hivyo, tutalifanyia kazi ili
kufahamu jinsi ya kulitatua,”alisema Hamad.
Akizungumzia changamoto hiyo ya mwingiliano wa ratiba za kazi za
taasisi hizo, Balozi Sefue alisema jambo hilo ni miongoni mwa
yatakayozingatiwa wakati wa kufanya uamuzi.
“Tutakapokuwa tunafanyia kazi suala hilo, tutazingatia hayo yote na
tutahakikisha kwamba hakutakuwa na mwingiliano wa aina yoyote,” alisema
Sefue.CHANZO: MWANANCHI.
Wednesday, 3 September 2014
Wafungwa waiomba Serikali kuwatafutia adhabu mbadala kupnguza msongamano
![]() |
| Nembo ya Jeshi la Magereza. |
Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo (Wafungwa) na Mahabusu wameiomba Serikali kutafutiwa adhabu mbadala za kutumikia jamii kwa wanafunzi wanaopatikana na hatia kwa makosa madogo madogo ili kupunguza msongomano wa wanafunzi pamoja na Mahabusu gerezani .
Wakizungumza katika ziara ya Mahakimu wa Mahakama huko kiinua miguu Kilimani Zanzibar mwanafunzi Muhammed Hamza kwaniaba ya wezake amesema katika kuzingatia haki za binaadam yako makosa mengi ambayo Serikali ingalikaa na kuyatizama upya na kuyatafutia adhabu zitakazolingana na makosa hayo.
Hamza aliyataja baadhi ya makosa hayo kuwa ni wizi wa mazao, kuku ambapo alitoa mfano wa nazi mbili mtu anawekwa rumande miezi sita wakati kifungo chake inawezekana ikawa miezi miwili na mengine kama hayo.
Mwanafunzi huyo alitaja kutokuwepo kwa usawa wa sheria na kudai kwamba mara nyingi kunakuwa na viashiria vya rushwa katika upatikanaji wa haki na chuo cha mafunzo ni sehemu ya asokuwa nacho na mwenye nacho hastahiki, Sheria kutizama upande mmoja na mwengine kutofanyakazi wakati sheria haina mkubwa.
Alisema kuhusu upatikanaji wa mwenendo wa kesi mara zinapomalizika kwa kesi bado limekuwa tatizo sugu na kuchukuwa muda mrefu na hata waombaji kukata tamaa ya kukosa haki zao za msingi kupitia Mhimili huo wa Mahakama.
Kuhusu utaratibu wa upatikanaji wa dhamana ya rufaa kwa wanafunzi (wafungwa) wanaohukumiwa adhabu gerezani kuwa bado ni shida kupatikana wakati sheria ipo mtuhumiwa anaweza kubaki njee hadi rufaa yake yake itakapomalizika.
Akizungumzia dhamana za kawaida kwa kesi zilizopo Mahakamani Washitakiwa waliopo Rumande wamedai kuwa upo ubaguzi kwa wazanzibari na wazanzibara na vigezo wanavyowekewa ni vile ambavyo vinalenga kuwapa adhabu na sio haki za kisheria zilivyo.
Muhammed Hamza akitoa baadhi ya mifano kuwa kutolewa dhamana kwa Mansoor Yussuf Himid kwa kosa aliloshitakiwa nalo na wengine kubaki mahabusu kwa makosa ya aina moja ni ubaguzi, kutakiwa wadhamini watumishi wa Serikali wakati mwengine kunawanyima haki watuhumiwa walio wengi ambao hawana jamaa ambao ni watumishi wa serikali.
Madai mengine yaliyotolewa ni kuchelewa kwa kuanza kwa kesi Mahakamani na Mahakimu kutofanyakazi siku za Ijumaa wakati Mahabusu wanateseka gerezani na utaratibu wa kuwaita mashahidi hauko mzuri na kuchangia kesi kuwepo kipindi kirefu.
Gangira Charles ambae ni Mahabusu alitilia mkazo suala la haki ya dhamana kwa watuhumiwa na kunukuu Nakala ya gazeti la Mwananchi lililoandikwa kesi ya aliyekuwa Waziri wa SMZ Mansoor Yussuf Himid kupewa dhamana kwa kosa aliloshitakiwa nalo na wengine kubaki mahabusu kesi nyengine ni kesi za dawa za kulevya ambazo watuhumiwa wanamaliza Miaka bila kesi zao kumalizika kwa wakati na watuhumiwa kukaa ndani zaidi ya mwaka mmoja.
Gangira alishauri kwa Serikali kuandaliwa utaratibu utakaowezesha kesi zikasikilizwa kwa wakati ili haki zipatikane kwa wenye haki tena kwa wakati na dhamana zikitolewa kisheria mrundikano gerezani utaisha na Serikali haitakuwa na mzigo wa kuhudumia watu ambao wanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya taifa kwa kufanyakazi na kulipia kodi.
Wanafunzi hao wa rumande wakizungumzia vitendo vya unyanyasaji dhidi ya Watuhumiwa wanapokamatwa na kufikishwa vituo vya Polisi wamedai kufanyiwa vitendo ambavyo haviendani na haki za binaadamu pamoja na kupoteza mali zao ambazo wanaziweka Polisi.
Gangira alisema kuwa vitendo vingine wanavyofanyiwa Polisi ni mateso bila ya kupatiwa matibabu wanapopata majeraha na vitendo vya udhalilishaji kinyume na haki za binaadamu.
Aidha wamemuamba mrajisi wa Mahakama kuandaa utaratibu wa Kamishna wa Polisi Zanzibar kutembelea gerezani na watendaji wake kusikia kilio chao ili kuweza kupatiwa ufumbuzi utakaosaidia kupatikana kwa haki.
Mahabusu hao kwa pamoja wametaja matarajio yao makubwa ya kufanyiwa kazi malalamiko yao ili kuona kilio chao cha muda mrefu kinaisha na sheria kufuata mkondo wake na wamesema hawana lengo la kujenga chuki kati ya watendaji hao na Mahakimu lengo lao ni kujenga misingi imara ya kuendeleza kazi zao.
Akijibu baadhi ya malalamiko ya Wanafunzi(Wafungwa) na Mahabusu Mrajis wa Mahakama Kuu Georg Kazi alisema ziara yao wamejifunza mambo mengi ikiwemo kuona hali halisi ya Wafungwa na Mahabusu wanavyoishi gerezani.
Mrajis alisema amepokea malalamiko yao na atayafanyia kazi ambapo kuhusu dhamana ya Mansoor kuwa imefunguwa mlango kwa watuhumiwa wengine kutumia kifungu cha 150(4) kuomba dhamana na wao waone Mahakama itafanyaje kutokana na kifungu hicho hakijawahi kutumiwa hapa Zanzibar na Mansoor ameanza na wengine wafanye.
Kuhusu malalamiko ya shutuma kwa Mahakimu na kujihusisha na vitendo vya rushwa na kutotenda haki ameahidi kulifanyia kazi kuyaondosha malalamiko hayo na suala la dhamana litaangaliwa, kupatikana kwa mwenendo wa kesi Proceed amesema tatizo ni miundombinu finyu kunachangia kuchelewa lakini tayari tatizo hilo linafanyiwa kazi.
Georg Kazi amewaomba kuisaidia Mahakama ili kuzimaliza changamoto ambazo zipo na kuonekana kuwa ni kero kwa jamii ambapo Wanafunzi(Wafungwa) na Mahabusu ndio wadau wakuu ambao wanazifahamu kasoro zilizokuwepo.
Amewataka kupeleka malalamiko yao wale ambao kwa muda mrefu kesi zao hazijatolewa hukumu na tayari zimemalizika na kwa muda hazijatolewa hukumu.
Awali Kamishna wa Vyuo vya Mafuzo Khalifa Haji Chum alisema ujio wa Mahakimu kutasaidia kuleta ufanisi na mashirikiano katika taasisi hizo muhimu ambazo zimebeba jukumu kubwa la kusimamia sheria za nchi.
Kamishna Khalifa amesema ziara za watendaji wanaohusika na moja ya majukumu yao kunasaidia kuona wapi kwenye mapungufu na kuyafanyiakazi ili kudumisha amani katika nchi ambayo ndio dira ya maendeleo.
Mapema Msaidizi Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo Haji Vuai Usi alisema wapo wanafunzi 169 na Mahabusu 234 wakiwepo mfungwa mmoja mwanamke na watano mahabusu, watoto watano.
Nao Mahakimu waliotembelea gereza kuu la Kiinua Miguu wamesema wamejifunza mambo mengi katika ziara hiyo na kuiomba serikali kutoa ushirikiano wa kutosha kwa taasisi hizi ili kupunguza au kuondosha kabisa matatizo yaliyopo ikiwemo miundombinu.
Ukawa watahadharishwa kutoharibu mjadala wa katiba
![]() |
| Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mh, Balozi Seif Ali Iddi. |
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, amesema hawatakubali kuona Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), unauchafua awamu ya pili ya mjadala wa kupatikana katiba mpya, kwani kamati 12 za bunge zimemaliza kazi zake vizuri.
Aliysema hayo wakati akiwahutubia wanachama wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Chiuyu, wilaya ya Manyoni mkoaniSingida.
Balozi Seif, ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, alisema wanalazimika kutoa tahadhari hiyo kwa vile tayari kuna taarifa kwamba umoja huo huenda ukarudi bungeni baada ya kuzungumza na Rais Kikwete.
Alisema nafasi yao ya kurudi isiwe sababu ya kuchafua awamu ya pili ya mjadala huo.
Alisma CCM itaendelea na msimamo wake wa kutetea mfumo wa serikali mbili kwa sababu wananchi wameshaelewa madhara ya mfumo wa serikali tatu.
Alisema inashangaza kuona baadhi ya watu kudai wajumbe wa CCM, hawajadili rasimu ya Jaji Warioba, wakati taratibu zinawaruhusu wajumbe kurekebisha palipokosewa.
Aidha alisema madai kuwa katiba inayotungwa ni ya CCM hayana ukweli kwa sababu wajumbe wengine kutoka kundi la 201 wanashiriki kujadili.
Alisema nia ya serikali ni kuona Tanzania inapata katiba iliyo bora na itakayowaunganisha wananchi.
Sitta amshambulia Kubenea bungeni
![]() |
| Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta. |
Sitta alikwenda mbali na kumfananisha Kubebea na
mchekeshaji wa mfalme huku akimtuhumu kuwa wapo wafadhili nyuma yake
katika hatua yake hiyo.
“Karne za nyuma, karne ya 15, 16 na 17 wafalme
kule Ulaya walikuwa na watu wao wanaitwa court jesters (wachekeshaji).
Eneo la mfalme lilikuwa kama mahakama halafu kuna mchekeshaji,” alisema.
“Sasa wafalme wa Ulaya walikuwa wanaajiri
wachekeshaji kwa malengo mawili. Moja ni kumsifia mfalme kwa kila kitu
na jingine ni kuwasema wote wale ambao mfalme anahisi ni wabaya wake.
“Kwa hiyo kuna watu wa aina hiyo, tunawaona hadi
sasa kama kina Kubenea, ni mchekeshaji wa mfalme tu. Yeye kuna mfadhili
na wafadhili wako nyuma yake.”
Alisema wafadhili hao wanamsogeza kwa sababu
wamemwona ana vipaji vya kufanya kazi kama hizo. Tuwaone nao kuwa kuna
njia nyingi za kupata riziki tuwasamehe tu waendelee na shughuli zao”.
Akijibu madai hayo, Kubenea alisema: “Nimemsikia
Sitta, lakini sijafahamu kama alikuwa anazungumzia kesi niliyofungua
mahakamani au kazi zangu za uandishi wa habari, lakini madai kwamba
natumika, yeye (Sitta) anajua kwamba sijawahi na sitawahi kutumika.
Ninafanya kazi zangu kwa uadilifu na uaminifu mkubwa kwa masilahi ya
umma.”
Alisema hata pale gazeti lake lilipokuwa
linamwandika Sitta vizuri si kwa sababu alikuwa amewalipa, bali wakati
huo alikuwa anasimamia haki na hata sasa anapomwandika upande wake wa
pili, ndiyo ukweli wa jinsi alivyo.
Kubenea alisema Sitta anapingwa wakati huu
kutokana na kitendo chake cha “kutumia Bunge la Katiba kunyofoa maoni ya
wananchi katika kazi takatifu iliyofanywa na Tume ya Jaji Warioba.”
Sitta ajipigia debe urais
Sitta alitumia nafasi hiyo kujibu hoja
zinazotolewa dhidi yake kuwa jinsi anavyoendesha Bunge Maalumu,
amepungukiwa sifa za kuwania urais mwaka 2015 huku akijipigia debe
kiaina katika nafasi kuwania nafasi hiyo.
Muda mfupi kabla ya Kamati 12 za Bunge hazijaanza kuwasilisha
taarifa za kuhusu Rasimu ya Katiba, Mwenyekiti huyo aliweka wazi kuwa
iwapo Watanzania watahitaji rais makini na mwadilifu mwaka 2015 basi
wamfikirie pia yeye.
Alisema watu wanaojaribu kumpima kama anafaa
kugombea urais 2015 kwa kuangalia yale yanayotokea katika Bunge Maalumu
la Katiba wanampima kwa hoja duni.
“Wengine wananikejeli, wanasema kwa shughuli hii
naonyesha sifai urais, mimi sijaomba urais. Naifanya kazi hii kama
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,” alisema Sitta na kuongeza: “Haya mengine
rafiki yangu Juma Duni Haji (Makamu Mwenyekiti wa CUF) ananipima kwa
hoja zilizo duni kabisa. Anajaribu kunipima eti... lakini nasema
wanaochagua rais ni wananchi. Inawezekana mwakani wananchi wa Tanzania
wakatamani mtu mzima, aliyetulia, asiyewaogopa wapuuzi, wakatamani hilo.
Kama watahitaji mtu makini, mwadilifu basi wajue tu kuna sisi wengine
tunaweza kufikiriwa kwa mambo kama hayo.”
Kuhusu Tume ya Warioba
Sitta alisema wananchi wengi wameonyesha shauku ya
wajumbe kuendelea na vikao vya Bunge Maalumu la Katiba tofauti na
inavyotangazwa.
“Makundi mbalimbali ya wananchi walioisoma rasimu
yamebaini ina upungufu kama sisi, ndani ya kamati zetu tumeona hivyo na
hilo siyo jambo la ajabu na wala si kupuuza kazi ya Tume,” alisema.
Sitta alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini
ya Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba ilifanya kazi yake vizuri lakini
kama ilivyo hulka ya mwanadamu hakukosekani upungufu.
“Tukumbuke kuwa Tume ilipokea maoni kutoka kwa
wananchi 334,000 na mabaraza zaidi ya 700.
Walichokileta ni tafsiri yao kuhusu maoni hayo, mnielewe vizuri,” alisema Sitta na kuongeza: “Walikaa wakachambua, mengine wakayaacha mengine wakayarekebisha. Ingekuwa kuleta maoni yote ingekuwa likitabu likubwa ambalo tusingeweza kulibeba.”
Walichokileta ni tafsiri yao kuhusu maoni hayo, mnielewe vizuri,” alisema Sitta na kuongeza: “Walikaa wakachambua, mengine wakayaacha mengine wakayarekebisha. Ingekuwa kuleta maoni yote ingekuwa likitabu likubwa ambalo tusingeweza kulibeba.”
Sitta aliwasihi wajumbe wanaoendelea na bunge hilo
kutofadhaishwa na matusi na kejeli wanazorushiwa huku akisisitiza kuwa
yuko imara na hayumbi.
Kauli hiyo ya Sitta imekuja wakati makundi
mbalimbali ya jamii wakiwamo wasomi, wanasiasa, viongozi wa dini na
wanaharakati wakipaza sauti kutaka Bunge lisitishwe. Msingi wa kutaka
kusitishwa kwa Bunge hilo ni kutaka kutafutwa kwanza kwa maridhiano kati
ya CCM na wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao
wamesusia Bunge hilo.
Wajumbe wa Ukawa walisusia Bunge hilo tangu Aprili
mwaka huu, wakipinga kitendo cha Bunge kuacha kujadili rasimu iliyobeba
maoni ya wananchi na kuingiza mambo mapya waliyosema yana nia ya kubeba
masilahi ya CCM.
CHANZO: MWANANCHI.
CHANZO: MWANANCHI.
Mjumbe Arfi arudisha hoja za Ukawa bungeni
![]() |
| Mjumbe wa Bunge Maalumu, Said Arfi. |
Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Mpanda Kati (Chadema), alilitikisa Bunge
hilo, alipowasilisha maoni ya wajumbe wachache wa Kamati Namba 10
inayoongozwa na Anna Abdallah.
Alisema wajumbe wengi wamependekeza marekebisho ya sura ya saba kwa
kuweka Makamu wa Rais watatu yaani mgombea mwenza, Rais wa Zanzibar na
Waziri Mkuu.
Hata hivyo, alisema wachache wamependekeza sura hiyo kubaki kama
ilivyopendekezwa kwenye Rasimu kwa sababu muundo wa serikali tatu
uliopendekezwa hauhitaji kuwa na makamu wa rais watatu wala ofisi ya
Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa Rasimu hiyo, Ibara ya 70 inasema kutakuwa na Serikali
ya Jamhuri ya Muungano itayokuwa na Rais, makamu na mawaziri wa Jamhuri
ya Muungano.
Tofauti na walio wengi ambao wamependekeza mawaziri na naibu mawaziri
watokane na Bunge, wachache katika kamati hiyo wametaka ibaki kama
ilivyo katika Rasimu ya kuwa mawaziri wasitokane na wabunge.
Alisema mapendekezo hayo yataleta ufanisi zaidi katika utendaji wa mawaziri katika wizara husika.
“Sababu nyingine ni kuondoa uwezekano wa waziri ambaye ni mbunge kupendelea jimbo lake la uchaguzi ili aweze kuchaguliwa tena katika chaguzi zinazofuata,” alisema.
“Sababu nyingine ni kuondoa uwezekano wa waziri ambaye ni mbunge kupendelea jimbo lake la uchaguzi ili aweze kuchaguliwa tena katika chaguzi zinazofuata,” alisema.
Pia alisema wajumbe wengi wameondoa dhana ya Serikali ya Tanganyika
na kufuta mapendekezo yanayoweka utaratibu wa viongozi wa serikali hiyo
kushiriki katika chombo cha uhusiano na uratibu wa Serikali
kinachoanzishwa na Rasimu.
Hata hivyo, alisema wajumbe wachache wamependekeza ibara hizo zibaki
kama zilivyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba kwa sababu maudhui
yaliyowekwa yanakidhi muktadha na majukumu ya chombo husika katika
muundo wa serikali tatu.
Arfi alisema wajumbe wengi walipendekeza kuingizwa kwa sura na sehemu
mpya zilizopendekezwa kuhusu mamlaka ya umma, ardhi, maliasili na
mazingira na sehemu ya Taasisi ya Kuzuia Rushwa katika sura ya 13.
Alifafanua kuwa wajumbe wengi pia walipendekeza sura ya ardhi, maliasili na mazingira.
“Wajumbe wachache hawazikubali sura na ibara mpya zote
zilizopendekezwa kwani zinalenga katika kuongeza mambo ya muungano
katika Rasimu ya Katiba,” alisema.
Katika kamati hiyo, wajumbe wengi wamependekeza kuwapo na uraia wa
nchi zaidi ya moja kwa sababu Watanzania walioko nje ya nchi wangependa
kurudi na kuwekeza nyumbani kwao.
Hata hivyo, alisema wajumbe wachache wamependekeza sura hiyo ibaki
kama ilivyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba kwa sababu kuna hatari
nyingi zinazoambatana na uraia pacha ikiwa ni pamoja na kuhatarisha
usalama wa nchi.CHANZO: MWANANCHI.
Tuesday, 2 September 2014
Sitta azidi kuinanga rasimu ya Jaji Warioba
![]() |
| Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta. |
Kutokana na hali hiyo, amesema Bunge Maalumu la Katiba limelazimika kuiboresha kwa kuwa kila kitu kinachoandikwa na binadamu hakiwezi kuwa sahihi.
Sitta alitoa kauli hiyo mjini hapa jana, alipokuwa akipokea ujumbe wa viongozi wa vyama na asasi za watu wenye walemavu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
“Kuna mambo yanaendelea hapa, wengine wanayakejeli, ingawa ni ya kawaida kuelekea kupata Katiba mpya.
“Jambo lolote lililoandikwa na binadamu haliwezi kuwa sahihi, hii rasimu siyo msahafu kiasi kwamba haiwezi kubadilishwa, hiyo siyo sahihi kabisa.
“Hao wanaosema tunafanya mambo ya tume, waendelee kusema tu, lakini Bunge Maalumu la Katiba lina mamlaka ya kurekebisha upungufu hata msemeje, rasimu hii tumegundua ina upungufu kadha wa kadha, lazima tuiboreshe.
“Bahati nzuri hata waandishi wengine mko hapa, yaani hata nyinyi mmeamua kujiingiza katika jambo hili hadi mnaandika ‘ma-editorial’.
“Kuna vita kubwa na nzito, kuna watu wanapiga vita taasisi hii, mimi siwajali, yaani sijawahi kuona watu wakikosa uzalendo kiasi hiki, lakini sisi tutaendelea hata mkifanyaje,” alisisitiza Sitta.
Pamoja na hayo, Sitta alizungumzia mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba na kusema linaendeshwa vizuri na kwamba Katiba mpya itakayopatikana itakuwa nzuri na wananchi wataifurahia.
“Kwa maana hiyo, ndugu zangu walemavu msiwe na wasiwasi, haya mnayoyasema hapa nitahakikisha yanaingizwa kwenye majumuisho, kwani hata leo mchana (jana) nitakutana na Kamati ya Uongozi ambayo nitaieleza juu ya haya mapendekezo yenu,” alisema.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ushauri cha Watu Wenye Ulemavu, Kaganzi Rutachwamagyo, aliwasilisha ripoti ya mapendekezo wanayotaka yawemo katika Rasimu ya Katiba mpya.
Katika mapendekezo hayo aliyosema yamesainiwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata), Felician Mkude, Rutachwamagyo alisema yamefanyika kwa sababu rasimu ya Katiba imezungumzia walemavu bila kuwaangalia kwa undani.
“Kuna msemo katika Biblia sijui uko sura gani na katika kitabu kipi, lakini unaeleza kwamba Yesu anasema hakuja kutengua Torati bali kuitimiliza.
“Kwa mfano, kifungu cha 113 cha Rasimu ya Katiba kinasema Rais atachagua watu wenye ulemavu watano kuwa wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini sisi tunaona hii siyo sawa kwetu,” alisema.
Mjadala wa jumla ndani ya Bunge Maalumu la Katiba unaanza leo kwa Kamati 12 za Bunge hilo kuwasilisha taarifa zao.
Mjadala huo unaanza wakati baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo wanaounda kundi la Ukawa wakiwa bado wamegoma kurudi, huku hofu kubwa ikitawala kama wajumbe waliobaki wataweza kupitisha Ibara za rasimu hiyo kwa kupata idadi ya theluthi mbili kwa kila upande wa Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013.
Subscribe to:
Posts (Atom)





