Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim, Seif Sharif Hamad. |
Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Serikali
ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, ameshikilia nafasi hiyo ya ukatibu mkuu
wa CUF kwa miaka 15 tangu mwaka 1999 alipoachana na cheo cha umakamu
mwenyekiti, na iwapo atapitishwa na mkutano huo atakuwa amekalia cheo
hicho kwa miaka 20 mfululizo.
Akitoa taarifa kuhusiana na mkutano mkuu wa sita
wa chama hicho unaotarajia kuanza leo Dar es Salaam, Mkurugenzi Haki za
Binadamu, Habari na Uenezi, Salum Biman alisema hakuna mwanachama
aliyejitokeza kupambana na Maalim Seif.
“Hiyo nafasi ilitangazwa mwezi mzima, lakini
hakuna mwanachama aliyejitokeza,” alisema na kuongeza;“Hata wewe
ungekuwa mwanachama wa CUF, ungekuwa na haki ya kugombea nafasi hiyo,
hakuna mwanachama aliyekatazwa.”
Kuhusu nafasi ya mwenyekiti, Biman alisema kuna
wanachama wawili wamejitokeza kupambana na Profesa Lipumba. Aliwataja
wagombea waliojitokeza kuwa ni Chief Lutayosa Yemba kutoka Shinyanga na
mwingine aliyemtaja kwa jina la Ibrahim kutoka Mkoa wa Pwani. Hata
hivyo, taarifa nyingine zimemtaja pia Mbezi Adam Bakar kutoka Temeke,
Dar es Salaam.
“Wagombea hao ndiyo watakaopambana na Profesa Lipumba katika nafasi ya uenyekiti,” alisema.
Kuhusu nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Bimani alisema
aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo, Machano Khamis ameachia ngazi na
kumpisha Waziri wa Afya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar,
Juma Haji Duni.
Alisema mkutano huo utawashirikisha wajumbe 800
kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na utafanyika kwa siku tano, unatarajia
kumalizika Juni 27, mwaka huu.
“Taarifa mbalimbali za chama zitasomwa baada ya
miaka mitano ya utendaji. Katika mkutano huo, mwenyekiti Profesa Lipumba
na katibu mkuu wake wataachia ngazi ili kupisha uchaguzi mkuu uweze
kufanyika.”
Aliongeza kuwa mkutano huo utateua pia wajumbe 45
wa Baraza Kuu kutoka kila kanda na wajumbe wanawake ambao ni asilimia 30
ya wajumbe wote wa mkutano mkuu.
“Hadi sasa Wilaya 10 za Zanzibar na 90 za Bara
zimeshakamilisha uongozi wa wilaya, hivyo zitatuwezesha kufanikisha
uchaguzi katika mkutano mkuu,” alisema.
Mbali na uchaguzi huo alisema mkutano huo utarekebisha baadhi ya vipengele vya katiba na kanuni za chama hicho.
Alisema baada ya uchaguzi wa kamati kuu, mwenyekiti kwa kushirikiana na makamu watateua wakurugenzi wa idara ambao watathibitishwa na Baraza Kuu kabla ya kupendekeza majina ya manaibu katibu ambao watathibitishwa na uongozi.
Alisema baada ya uchaguzi wa kamati kuu, mwenyekiti kwa kushirikiana na makamu watateua wakurugenzi wa idara ambao watathibitishwa na Baraza Kuu kabla ya kupendekeza majina ya manaibu katibu ambao watathibitishwa na uongozi.
No comments:
Post a Comment