Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. |
Na Othman Khamis
Ame - OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Seif Ali Iddi ameonya kuzuiwa kufanywa kwa ujenzi wa aina wowote katika eneo la
Masoko makongwe liliopo Mtaa wa Selemu ndani ya Mji wa Wete hadi Serikali Kuu
itakapotoa maamuzi yake.
Balozi Seif alitoa onyo hilo mara baada ya
kuliangalia eneo hilo lililoleta mgogoro baina ya Uongozi wa Baraza la Mji Wete
pamoja na Wafanyabiashara wa soko hilo dhidi ya mfanyabiashara Ahmed Abdulla
Mapete aliyeuziwa sehemu hiyo na baadhi ya watendaji wa Baraza la Mji Wete
kinyume na taratibu za Serikali.
Alisema Serikali ilitenga eneo hilo maalum
kwa ajili ya huduma za soko ili litoe huduma kwa wakaazi wa Mji huo tokea mwaka
1942. Hivyo amewaagiza wafanyabiashara wanaoendesha biashara zao katika sehemu
hiyo waendelee kama kawaida hadi Serikali Kuu itakapotoa maamuzi kutokana na
mgogoro huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alimekea vitendo vya baadhi ya watumishi wa umma wanaoamua kujichukulia maamuzi
mikononi mwao kinyume na taratibu zilizowekwa na Serikali na hatua za
kuwawajibisha hazitochelea kuwachukulia dhidi ya watumishi hao.
“ Hili ni soko lililotengwa na Serikali
kwa ajili ya kuwajengea mazingira wananachi kupata huduma za msingi za mahitaji
yao ya kila siku. Sasa hii tabia ya baadhi ya watendaji kujichukulia maamuzi
kwa kuzitelekeza mali za Serikali wamepewa amri na nani ? “ Alikemea Balozi
Seif.
Balozi Seif alisema kwamba mtu ye yote
atakayeamua kuuza eneo la Serikali bila ya idhini ya Taasisi inayohusika na
masuala ya ardhi aelewe kwamba anafanya makosa na Serikali haitakuwa tayari
kulipa fidia endapo mali au jengo aliloiweka katika ardhi hiyo itaondoshwa.
Alifahamisha kwamba mgogoro wa soko kongwe
la Selemu Wete tayari unaeleweka Serikalini na muda si mrefu maamuzi rasmi ya
suala hilo la muda mrefu yatatolewa kwa mujibu wa sheria na taratibu za
Serikali.
No comments:
Post a Comment