Rais wa Tanzania Dk Kikwete akiwa na Rais wa Zanzibar Dk Shein |
Duni ambaye pia ni kiongozi wa CUF, alisema hayo
jana kwenye mdahalo kuhusu Bunge Maalumu la Katiba tunayoitaka
uliofanyika Dar es Salaam.
“Ngoma hiyo imeshakwama, kamwe haturudi bungeni
kujadili mambo ya CCM kwani hayatuhusu. Kwa mazingira yaliyopo, ule sasa
umegeuka kuwa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM, wanaweka mambo yenye
masilahi kwa chama chao, kamwe haturejei,” alisema.
Alisema kama viongozi hao hawazioni dosari
zinazofanywa na wajumbe wa CCM, basi suala la kupata Katiba Mpya ni
ndoto kwa sababu Ukawa hawako tayari kurejea katika Bunge hilo.
“Tunawaachia CCM waandae Katiba ya Watanzania, sisi hatutashiriki kwa sababu tumegundua rafu hiyo mapema,” alisema.
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar,
Vuai Ali Vuai alisema hata kama Ukawa hawatarejea bungeni, vikao
vitaendelea kama kawaida kwa sababu kanuni zinawaruhusu kufanya hivyo.
“Katika Bunge Maalumu la Katiba, wapo wabunge wa
CCM na wale 201. Walioteuliwa na Rais ambao walitoka nje pamoja na Ukawa
ni wajumbe 25 na wamebaki 176, hivyo watu wasiseme waliobaki ni wajumbe
wa CCM,” alisema.
Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Marekebisho ya Katiba,
Humphrey Polepole alisema Bunge Maalumu la Katiba halina mamlaka ya
kubadilisha rasimu hiyo, bali kuiboresha.
CHANZO: MWANANCHI.
CHANZO: MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment